STARS KUKWEA PIPA LEO KUELEKEA MISRI.. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Tuesday, 30 May 2017

STARS KUKWEA PIPA LEO KUELEKEA MISRI..Kikosi cha timu ya tafifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea mjini Alexandria kwaajili ya kambi ya wiki moja ili kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaopigwa tarehe 10 mwezi ujao.

Hayo yamethibitishwa na Rais wa shirikisho la kandanda nchini Mh Jamal Malinzi kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo ameandika "Taifa Stars itaondoka leo kuelekea Alexandria Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya Afcon vs Lesotho tar 10/06"

Kikosi hicho kinachofundishwa na Kocha Salum Mayanga kinaundwa na makipa Aishi Manula  (Azam FC), Benno Kakolanya  (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe    (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael.

Walinzi wa kati Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye hatasafiri na timu kwa sasa.

Viungo wa kushambuliaji Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla  (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).

Na washambuliaji  Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting).

No comments:

Post Bottom Ad

Pages