SINGIDA UNITED YAVITISHA VILABU VYA SIMBA,YANGA NA AZAM MSIMU UJAO LIGI KUU TANZANIA. - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 27 May 2017

SINGIDA UNITED YAVITISHA VILABU VYA SIMBA,YANGA NA AZAM MSIMU UJAO LIGI KUU TANZANIA.Katika kujiandaa na msimu wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 timu mbalimbali zimekua zikifanya maandalizi yaliyojitosheleza ili kuhakikisha  haziendi kushiriki tu bali kutoa upinzani na hata kutwaa ubingwa.

Moja ya timu ambazo hadi sasa zimekua tishio kwa vigogo wa ligi hiyo hasa kwenye usajili ni timu ya Singida United ambayo hadi sasa imekwisha kufanya usajili wa nyota mbalimbali wakiwemo wa nje ya nchi na kuvifanya vilabu vikubwa nchini kama vile Simba,Yanga na Azam kutishika.

Mpaka sasa klabu hiyo imekwisha kuwasajili wachezaji kadhaa na hawa hapa ni baadhi yao.Elisha Muroiwa,Wisdom Mtasa,Tafadwaza Kutinyu,Shafik Batambuze ,Simbrashe Nhivi na Kenny Ally ambae vilabu kadhaa vya hapa nchini pia vilikua vikimuwani..

No comments:

Post Bottom Ad

Pages