MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI, POLE SIMBA SC - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 29 May 2017

MALINZI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI, POLE SIMBA SC


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu rambirambi kwa Rais wa Klabu ya Simba ya Dar es Salaam, Evans Aveva kutokana kifo cha shabiki wa timu hiyo, Shose Fedeline aliyefariki dunia jana mchana Mei 28, 2017 katika ajali ya gari.

Kadhalika, Rais Malinzi ametuma salamu za pole kwa majeruhi katika ajali hiyo akiwamo Nahodha wa Simba, Jonas Mkude na dereva wa gari hilo ambalo lilikuwa safarini kurejea Dar es Salaam kutoka Dodoma. “Nakuandikia Rais wa Simba, Bw. Evans Aveva, pia ndugu, jamaa na marafiki pamoja na majirani wa marehemu Shose Fideline na wanafamilia wengine wa mpira wa miguu, kwamba nimepokea taarifa za ajali ya gari iliyosababisha kifo cha mmoja wa mashabiki wa timu ya Simba kwa masikitiko makubwa sana. Wito wangu, nawaomba wanafamilia wote kuwa watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Rais Malinzi.

Imetolewa na TFF..

No comments:

Post Bottom Ad

Pages