KOCHA LWANDAMINA AMTAKA HUYU KUTUA JANGWANI MSIMU UJAO - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Saturday, 27 May 2017

KOCHA LWANDAMINA AMTAKA HUYU KUTUA JANGWANI MSIMU UJAO

Kocha  wa Kagera Sugar Meck Maxime amefunguka Kuwa Kocha wa Yanga George Lwandamina ameonyesha nia ya Kufanya kazi naye, Haijaeleweka moja kwa moja kama atafanya naye kazi kama kocha msaidizi au atakuwa kwenye Benchi lake la Ufundi.

Maxime alisema

“Baada ya mechi yetu na Yanga ya msimu uliopita dhidi ya Yanga, kocha wao, Lwandamina alichukua mawasiliano yangu ambapo baadaye tulikutana na kuzungumza juu ya mambo mbalimbali lakini kubwa ni namna ya kujiunga na timu yao kwani anataka kufanya kazi na mimi.

“Licha ya kuongea huko, lakini mimi ni kocha siwezi kusema kwamba nitajiunga na timu fulani, lolote linaweza kutokea endapo tu tutakubaliana kwa vitu ambavyo nitakuwa navihitaji kwani huko nyuma nilishatoka Mtibwa na kwenda Kagera na hakutakuwa na maajabu kutoka hapa na kutua ndani ya timu hiyo,” alisema Maxime.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages