ATUPELE HUYOO SINGIDA UNITED - VYANKENDE.COM

Breaking

Post Top Ad

Millionaire  Ads

Monday, 29 May 2017

ATUPELE HUYOO SINGIDA UNITED


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Atupele Green, yupo mbioni kuingia mkataba wa miaka miwili katika timu ya Singida United kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Mchezaji huyo ambaye kwenye msimu uliomalizika hivi karibuni alikuwa kwenye kikosi cha JKT Ruvu, tayari yupo kwenye mazungumzo ya mwisho na uongozi wa Singida kwa ajili ya kusaini mkataba huo.

Akizungumza na BINGWA jana, mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usajili ya Singida United, alisema mchezaji huyo ni miongoni mwa matakwa ya kocha wao Hans van der Pluijm ambaye anavutiwa sana na mchezaji huyo.

Alisema usajili wa mchezaji huyo utakuwa ni wa pili kwa wachezaji wa ndani baada ya wiki iliyopita kuingia mkataba wa miaka miwili na mchezaji wa zamani wa Mbeya City, Kenny Ally.

“Atupele atasaini mkataba wa miaka miwili muda si mrefu, kwani tayari tumeshafanya naye mazungumzo kilichobaki ni kuingia mkataba huo na mchezaji huyo atakuwa wa pili kwa wachezaji wa ndani baada ya hivi karibuni kumsainisha Kenny Ally,” alisema mtoa habari huyo.

No comments:

Post Bottom Ad

Pages